Ubora mdogo katika huduma za afya Marekani

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maelfu ya watu hupoteza maisha kila mwaka kutokana na huduma za vya afya kuwa na ubora mdogo kulinganisha na viwango vinavyotakiwa

Ubora mdogo katika huduma za afya Marekani

Kutokana na viwango duni katika sekta ya afya nchini Marekani, Maelfu ya watu hufariki kila mwaka.

Katika habari iliyoenezwa na ukurasa wa intaneti wa Axios. Mwaka uliopita Marekani ilitumia dola trioni 3.5 katika sekta ya afya, Utafiti uliofanywa katika sekta ya afya unaonyesha kuna tatizo la viwango.

Nchini Marekani kwa mijibu wa sheria iliowekwa  inabidi katika kila hospitali 3, 1 itoe huduma ya dharura. lakini sheria hiyo inavunjwa , hilo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa ushirikiano wa WebMD na Georgia Health News. Pia kwa mujibu wa vyanzo vya habarivya ndani idadi ya vifo vya watoto katika hospital ya watoto ya John Hopkins ya Florida, imeongezeka viwango vya kushtusha.

Katika jimbo la Detroit hospitali moja imepatikana inatumia vifaa vya upasuaji ambavyo havikuwa visfi . Pia imefahamishwa kwamba hospitali za wagonjwa wa akili nchini humo zimekuwa huduma isiyotosheleza.

Kwa mujibu wa watoa habari hii,Mkurugenzi wa  shirika linapima ubora wa viwango vya huduma inayotolewa "Leapfrog Group" Leah Binder amesema kwamba kutokana na  kiwango cha ubora kinachotazamiwa kufikiwa  hakifikiwi kila mwaka maelfu ya watu hupoteza maisha kwa sababu ambazo zingeweza kuzuilika. Habari Zinazohusiana