HFPA kushirikisha wanachama wenye asili ya Kiafrika

HFPA yatangaza kutoa ushirika kwa wanachama wenye asili ya Kiafrika baada ya kukoselewa

1591843
HFPA kushirikisha wanachama wenye asili ya Kiafrika

Shirika la Golden Globe Awards ambalo hutoa Tuzo za Dunia, limetangaza kwamba litatoa ushirika kwa watu wenye asili ya Kiafrika baada ya kukosolewa kwa ukosefu wa wanachama kutoka sehemu tofauti.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Chama cha Waandishi wa Habari wa Kigeni wa Hollywood (HFPA), ambacho kimekuwa kikitoa Tuzo za Dunia kwa wasanii wa sinema na runinga kila mwaka tangu 1944 nchini Marekani kupitia Golden Globe Awards,  iliripotiwa kuwa "mpango huo wa utekelezaji" ulikuwa tayari.

Shirika la HFPA lenye makao makuu yake Kusini mwa California, hivi sasa lina washiriki 87, ambao wengi wao ni wanawake.

Wanachama wa shirika hilo wanajumuisha waandishi wa habari wa kimataifa ambao huripoti sinema na vipindi vya runinga ulimwenguni.

Inajulikana kuwa shirika la HFPA halijawahi kuwa na mwanachama yoyote mwenye asili ya Kiafrika kwa miaka 20 iliyopita.Habari Zinazohusiana