Je wajua

Ngano bora zaidi ulimwenguni

1574257
Je wajua

Je! Unajua kwamba "ngano ya einkorn"( ngano punje moja) , ambayo inakubaliwa kama ngano bora zaidi leo, ilipandwa Kusini mashariki mwa Anatolia miaka elfu 10 iliyopita?

Ngano hii, ambayo inasemekana kulimwa miaka elfu 12 iliyopita kulingana na baadhi ya vyanzo na miaka elfu 10 iliyopita kulingana na vyanzo vingine, inachukuliwa kama ngano bora zaidi ya kisasa tunayotumia leo. Ngano hii ambayo Kwanza ililimwa katika Kusini-Mashariki mwa Anatolia, leo hii imepandwa kwa wingi katika eneo la Kastamonu nchini Uturuki.

Ngano ya Einkorn, ambayo ililimwa na Wahiti na Wafurigia, iliitwa kwanza "Zız", ambalo ni neno la Wahiti, lakini baada ya muda neno hili likageuka kuwa siyez kwa lugha ya kituruki. Kipengele muhimu zaidi kinachotofautisha ngano hii na aina zingine za ngano ni kwamba haijawahi kuharibika kwa miaka elfu 10.

Siyez, ambayo ni ngano yenye glukosi ya chini, ina vitamini A zaidi, iron, asidi ya folic na zinki kuliko ngano ya kisasa. Kuna tafiti nyingi zinazoonyesha kuwa einkorn, ambayo pia ni rahisi kumeng'enya, ni faida zaidi kwa suala la afya.


Tagi: #ubora , #ngano

Habari Zinazohusiana