Utamaduni wa chai kwa Waturuki

Je wajua mtindo wa kupika na kuandaa chai ya Kituruki?

1470531
Utamaduni wa chai kwa Waturuki

Je wajua mtindo wa kupika na kuandaa chai ya Kituruki?

Chai, ambayo ina historia ya miaka 5000, iliingia katika maisha ya Waturuki na kutengeneza utamaduni wa kipekee katika jamii ya Kituruki.

Maeneo ya Karadeniz n Rize ni mashuhuri kwa aina mbalimbali za chai nchini Uturuki. Chai kutoka maeneo haya mara nyingi hujulikana kama chai ya kituruki.

Walakini, neno "chai ya Kituruki" hutambuliwa kwa jinsi inavyopikwa na kuandaliwa.

Ingawa kuna aina tofauti za chai na njia za kuandaliwa,Chai ya Kituruki hupikwakwa mtindo wake maalumu na hugawiwakatika vikombe vidoo vyembamba vya glasi.

Katika kutengeneza chai ya Kituruki, sufuria mbili hutumiwa.Moja inawekwa juu na nyingine chini kwa mtindo wa kubebana.

Sufuria ya juu huwekwa majani makvu na sufuria ya chini hutiwa maji.

Wakati maji yakiwa yanachemka,mvuke wake unakuwa unaingia katika majani yale makavu.Baadaye maji hayo yaliyochemka humimininwa kidogo katika sufuia la majani na kuacha yaendelee kuchemka.Inasubiriwa kama dakik kumi n chai yako inakuwa tayari.

Kwakuwa ni masufuria mawili la juu lenye chai yenyewe na la chini lenye maji ya moto, utayarishaji wa chai hufanywa kwa kumimina kiasikutoka sufuria ya juu na kiasi kutoka sufuria ya chini kulingana na mtu atakavyotaka kunywa.

Kwa wale wapendao chai yenye majani mengi basi hujaziwa glasi zao kutoka sufuria ya juu na maji kidogo kutoka sufuria ya chini. Na kwa wale wapendao chai yenye majani kidogo basi huwekewa chai kidogo na maji mengi.

Sukari huwekwa pembeni kwa atakayetaka kutumia.

Chai ni moja ya masoko makubwa nchini Uturuki.

Chai ni muhimu katika maisha na utamaduni wa Kituruki. Wakati huo huo, tamaduni ya chai ni moja ya ishara muhimu zaidi za maisha ya kawaida na ukarimu wa Waturuki.

 Habari Zinazohusiana