Msanii kutoka Burundi azua gumzo  baada ya kuomba anunuliwe gari

Msanii nchini Burundi anaejulikana kwa jina la Mr. Champagne amezua gumzo kwa wapenzi wa muziki na sanaa baada ya kusambaza video ikiomba mchango anunuliwe gari

1421052
Msanii kutoka Burundi azua gumzo  baada ya kuomba anunuliwe gari


Msanii nchini Burundi anaejulikana kwa jina la Mr. Champagne amezua gumza kwa wapenzi wa musiki na sanaa baada ya kusambaza video ikiomba mchango anunuliwe gari.

Mr. Champagne ni Msanii kutoka nchini Burundi ambae alijibatia umashuhuri  kwa kutoa vibao kadhaa ikiwemo kibao kilitamba kwa jina la "Qu'est ce qu'il ya",  maneno ya kifaransa ambayo yanatafsiriwa kwa kiswahili kwa "Nini unataka? " au "Kuna nini au Tatizo lako nini" .

Msanii huyo amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuzagaa kwa video yake  ambao anaonekana akishuka kutoka katika  usafiri aina ya  Bajaji na  kuwatolea wito mashabiki zake wamkusanyie fedha aongeze katika kiwango cha fedha alichokipata baada ya kusaini mkataba ili aweze kununua gari.

Mr. Champagne amewaomba mashabiki zake  kulingana na uwezo wao kila mmoja kutoa kiwango cha pesa anachoweza ili aweze kununua gari kwa kusema kuwa  amechoka kutembelea pikipiki na Bajaji yeye kama msanii anaewakosha nyoyo zao.

Kwa mujibu wa Msanii huyo, ni aibu  kwao Msani kama yeye  kuingia katika tamasha  akiwa anatumia aina hiyo ya usafiri.

Katika mahojiano aliofanya na kitengo kinachohusika na utamaduni , Mr. Champagne ametueleza kuwa anashangazwa na watu wanaomkejeli kutokana na ombi lake hilo  huku akisema kuwa msaada huo amewaomba mashabiki zake.

Kupitia ukurasa wake katika mtandoa wa kijamii wa Instagram , alizungumza moja kwa moja na mashabiki zake ambao walionesha mitazamo tofauti kuhusu ombi lake.

Kampeni ya kukusanya pesa ili awezekununuliwa gari inaendelea.
 Habari Zinazohusiana