Mcheza filamu maarufu wa hollywood, Kirk Douglas afariki dunia

Kirk Douglas, mcheza filamu kutokea Hollywood afariki dunia akiwa na umri wa miaka 103

Mcheza filamu maarufu wa hollywood, Kirk Douglas afariki dunia

Mcheza filamu maarufu kutoka Marekani, Kirk Douglas amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 103.

Mtoto wa kiume wa  muigizaji huyo maarufu, Michael Douglas, ametangaza kifo cha baba yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika taarifa yake Douglas alisema,

“ Mimi na ndugu zangu kwa tunasikitika kuwatangazia  kwamba Kirk Douglas ametutoka leo akiwa na umri wa miaka 103”.

Kirk Douglas ni mmoja wa wacheza filamu mashuhuri kupata kutokea Hollywood, amecheza filamu mbalimbali kama vile , "Spartaküs", " Paths of Glory ", " 20,000 Leagues Under the Sea " na  "Champion".

Douglas amewahi kutajwa kuwania tuzo za Oscar mara 3, na mwaka 1996 alishinda tuzo hizo.

 Habari Zinazohusiana