Billie Eilish avunja rekodi tuzo za Grammy

Mwanamuziki Billie Eilish (18) avunja rekodi tuzo za Grammy, aondoka na tuzo tano

Billie Eilish avunja rekodi tuzo za Grammy
62. grammy odulleri4.jpg
62. grammy odulleri3.jpg
62. grammy odulleri2.jpg
62. grammy odulleri1.jpg
62. grammy odulleri.jpg

Mwanamuziki Billie Eilish (18) avunja rekodi katika tuzo maarufu za muziki duniani za Grammy, hiyo ni baada ya kunyakua tuzo za rekodi bora bora ya mwaka, albamu ya mwaka, wimbo bora wa mwaka na tuzo nyingine ikifanya aondoke na tuzo 5 usiku huo.

Washindi wa tuzo za 62 za Grammy wapatikana katika tafrija iliyofanyika huko Los Angeles.

Mwongozaji wa sherehe za tuzo hizo alikuwa ni mwanamuziki wa Marekani Alicia Keys, katika ufunguzi wa sherehe hizo nguli wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant aliepoteza maisha katika ajali ya helikopta alikumbukwa.

Mwanamzuiki wa Pop  Lizzo, akifanya onyesho la kwanza la usiku huo alianza kwa kusema “Usiku huu ni kwa ajili yako Kobe”

 Michelle Obama mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama naye alijanyakulia tuzo ya “albamu bora ya maneno”usiku huo kupitia toleo la sauti la kitabu alichokiandika “Becoming”.Habari Zinazohusiana