Hawa ndio wasanii wa muziki waliotengeneza mpunga mrefu zaidi Spotify

Drake aongoza orodha ya wasanii waliosikilizwa zaidi kupitia Spotify katika kipindi cha miaka 10

Hawa ndio wasanii wa muziki waliotengeneza mpunga mrefu zaidi Spotify

Spotify kampuni yenye makao makuu yake nchini Sweden, inayojihusisha “podcast” na kuuza muziki kimtandao limetangaza kwamba msanii aliyesikilizwa zaidi kwa kipindi cha miaka 10 ni Drake.

Drake mwanamuziki na muigizaji kutoka Canada katika Spotify amesikilizwa mara bilioni 28 akiwa ndio msanii aliyesikilizwa zaidi. Ngoma ya Drake ya "One Dance" ilisikilizwa mara bilioni 1.7.

Katika miaka 10 ya hivi karibuni takwimu zinaonyesha kwamba Drake anafuatiwa na Muingereza Ed Sheeran, Rapa kutoka Marekani Post Malone, muigizaji na muimbaji raia wa Marekani, Ariana Grande, na rapa wa Marekani, Eminem.

Katika ngoma zilizosikilizwa zaidi miaka ya 2010 Spotfy wamefahamisha kwamba namba 1 ni "Shape Of You” wa (Ed Sheeran) namba 2 ni "One Dance Drake" (Drake), namba 3 ni "Rockstar" (Post Malone), namba 4 ni "Closer" (The Chainsmokers) na namba 5 ni  "Thinking Out Loud" wa (Ed Sheeran).

Ilifahamishwa kwamba wimbo "Shape Of You" ulisikilizwa mara bilioni 2,4.

Kwa mujibu wa Spotify ngoma iliyosikilizwa zaidi mwaka 2019 ni "Senorita" ya kwake Shawn Mendes na Camila Cabello.

Katika orodha ya nyimbo zilizosikilizwa zaidi mwaka huu baada ya "Senorita" zinafuatia "Bad Guy" (Billie Eilish), "Sunflower" (Post Malone), "7 Rings" (Ariana Grande) na "Old Town Road" (Lil Nas X).


Tagi: Drake , Spotify

Habari Zinazohusiana