Nyumba ambayo Shake Spear alindika Romeo na Julieta yatambuliwa

Mtafiti agundua nyumba ambayo Shake Spear aliishi kati ya mwaka 1597 na 1598

Nyumba ambayo Shake Spear alindika Romeo na Julieta yatambuliwa

Nyumba ambayo mtunzi wa mashairi na michezo ya kuigiza maarufu wa Uingereza, William Shake Spear aliaandaa moja ya kazi yake maarufu kabisa ya Romeo na Julieta yafahamika.

Shirika la habari la uingereza la BBc limeripoti kwamba , mwanahistoria wa sanaa za kuigiza, kwa kulinganisha dalili mbalimbali ameweza kubaini nyumba iliyopo jijini London  ambayo Shakespear aliishi kipindi cha mwaka 1597 na 1598.

Marsh ambaye aliendesha utafiti huo kwa muda wa karibu miaka 8 alibaini kwamba Shake Spear aliishi mashariki mwa London katika mtaa wa Bishopgate barabara ya Great St Helen nyumba namba 35.

Nyumba hiyo ambapo ndipo mchezo wa kuigiza wa Romeo na Julieta ulitungwa kwa hivi sasa ni eneo la kiofisi.Habari Zinazohusiana