Watalii kutoka Balkans wafurika  mkoani Edirne Uturuki

Mkao wa Edirne Uturuki washika nafasi ya tatu kuwa na watalii wengi mwaka 2018

1173734
Watalii kutoka Balkans wafurika  mkoani Edirne Uturuki

Mkoa wa Edirne nchini Uturuki umeshika nafasi ya ya tatu kwa kupokea watalii milioni 3 mwaka 2018.

Mkoa wa Edirne umeshika nafasi hiyo baada ya jiji la Istanbul na Antalya.

Jiji la Edirne linaendelea kuwavutia watalii kutokana na madhara yake na  hali yake ya hewa mabyo ni ya kipekee.

Watalii kutoka nchini Ugiriki na Bulgaria na mataifa mengine eneo la Balkans wanazidi kuingia nchini Uturuki.

Katika kipindi hiki ambacho msima wa baridi unamalizika, watalii kutoka  nchini  Rumania, Kroatia, Makedonia na Serbia wameingia kwa wingi nchini Uturuki.

Zaidi ya watalii 20000 kutoka Ugiriki na Burgaria wameingia Uturuki  mwishoni mwa wiki.Habari Zinazohusiana