Uturuki na Utalii

Uturuki na Utalii, mskiti wa Selimiye

1151873
Uturuki na Utalii

 

Mskiti wa Selimiye unaopatikana nchini Uturuki ni kazi muhimu na mashuhuri iliochwa na mbunifo katika sana aya ujenzi Sinan ambae ni miongoni mwa  wakandarasi na mafundi ujenzi mahiri katika historia na historia ya ujenzi.

Mskiti huo wa Selimiye ni mmoja miongoni mwa  miskiti  na majengo muhimu  ya kihistoria nchini Uturuki. Ni moja  katika majumba na majengo  ya kihistoria yaliojengwa katika kipindi cha utawala wa dola ya Uthamnia na Uturuki ulimwenguni.

Mskiti wa Selimiye ulijengwa katika karne ya 16 mkoani Edirne, mji mkuu katika kipindi cha utawala wa Dola  ya Uthmania kabla ya kudhibiti Istanbul.

Ni moja ya kazi ya kiufundi na ujenzi zilizoachwa na utawala wa dola ya Ottoman na  mhandisi Sinan.

Ujenzzi wa mskiti huo ulitolewa amri na mfalme Sultan Selim wa Pili amabe alisema kuwa jengo hilo iwe miongoni mwa majumba  ya kisitoria  kwa teknolojia ambayo ilitumika katika ujenzi wake na katika kipindi ambacho  teknolojia haikuwa  kama ilivyo leo.

Ujenzi wa mskiti huo  umevutia  watu wengi waliotembelea jengo hilo katika historia. Ujenzi wake umeanza mwqaka 1568 na kumalizika mwaka 1575 na mufundi zaidi ya 15 000 walikuwa  wakiwajibika kama ilivyotakiwa.

Kwa mabali, jengo la mskiti huo linavutia na kushangaza zaidi pindi utakapokuwa umeingia  katika jengo la mskiti. Ujenzi wake unashangaza kutokana na usawa wake  na  sheria za ujenzi katika kipindi hicho ambazo hadi leo bado wahandisi wanajaribu kuelewa. Mhandisi Sinan alikuwa hodari katika ujenzi. Licha  ya kuwa na paa kubwa , hakuna  kiguzo ambaco kinauzuia  paa hilo ambalo limewekwa kitaalmu.

Mskiti huo una eneo ambalo lina uwezo wa kupokea waumini zaidi ya 6 000 na kuendesha ibada kwa utulivu.  Minara yake  inapatikana katika pembe nne za mskiti.

Mhandisi Sinan ameacha kazi kubwa  ambayo kşhistoria inaupa hadhi utwala wa Ottoman katika sekta ya ujenzi. Marumaru, mbao za  thamani zimetumiwa kawa marembo ya ndani ya mskiti huo wa Selimiye mkoani Edirne.Habari Zinazohusiana