Serikali ya Afrika kusini kutambua ndoa za kiislam

Mahakama imeitaka serikali kutunga sheria ndani ya miezi 24 itakayohusiana na ndoa za kiislam

Serikali ya Afrika kusini kutambua ndoa za kiislam

Siku ya ijumaa mahakama nchini afrika kusini ilitoa uamuzi na kuitaka serikali kutambua ndoa za kiislam na kutunga sheria ambayo itasimamia ndoa hizo.

Mahakama kuu ya western cape imetoa uamuzi huo kufuatana na  shauri lililowekwa na kituo cha wanawake na sheria, shauri hilo lilikua linalenga kuwapa kinga ya kisheria watoto na wanawake wa kiislam wakati wa kutalikiana kwa wanandoa.

Shaykh Riad Fataar ambaye ni makam wa rais wa baraza la sheria la kiislam la nchini afrika kusini amesema kuwa uamuzi huo wa kutambua ndoa za kiislam ni mafanikio kwa waislam wote nchini ambao ni jamii ya wachache. Afrika kusini ina jumla ya watu milioni 55 kati ya hao waislam ni asilimia 1.5 tu.Habari Zinazohusiana