"Hamam" ya kihistoria yahamishwa nchini Ututuki

Sehemu ya kuogea ya kitamaduni ya waturuki ijulikanayo kama "Hamam" imehamishwa nchini Ututuki.

"Hamam" ya kihistoria yahamishwa nchini Ututuki

Sehemu ya kuogea ya kitamaduni ya waturuki ijulikanayo kama "Hamam" imehamishwa nchini Ututuki.

Hamam hiyo iliyojengwa karne ya 13 imehamishwa kutoka katika mji wa kihistoria wa Hasankeyf kutokana na ujenzi wa bwawa.

Kwa mujibu wa habari,sehemu hiyo ya kuogea imehamishwa kilomita 3 kutoka ilipokuwa hapo awali kwa lengo la kuilinda isifurike pale bwawa jipya litakapofunguliwa.

Gavana wa Batman Ahmet Deniz amesema kuwa majengo mengine 6 ya kihistoria yatahamishwa na Hasankeyf itaitunza historia yake.

Hasankeyf ilitangazwa kuwa sehemu ya kihistoria toka 1981. Kuna karibu mapango 6,000 katika eneo ambalo lina historia ya Byzantine, Kikristo na Kiislamu.

 Habari Zinazohusiana