Mradi wa kituo cha utamaduni cha Atatürk wazinduliwa mjini Istanbul

Rais Erdoğan asema kuwa Uturuki ni taifa lenye utajiri mkubwa wa kitamaduni

841768
Mradi wa kituo cha utamaduni cha Atatürk wazinduliwa mjini Istanbul

 

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğana asema kuwa Uturuki ni taifa ambalo lina utajiri mkubwa wa kitamaduni wakati mradi wa kituo cha utamaduni cha Utatürk kikizinduliwa.

Uzinduzi wa kituo hicho umefanyika mjini IStanbul.

Katika uzinduzi huo, mradi hupo umefafanuliwa kwa kina na rais Erdoğan amesema kuwa Uturuki ni taifa ambalo lina utajiri wa kipekee wa kitaduni.

Uturuki ina utajiri mkubwa kutoka Mashariki, Asia ya Kati, Caucase na maeneo mengine. Utamaduni wa Mesopotamia unapatika Kusini-Mashariki mwa Uturuki.

Rais Erdoğan amewaambia walioshiriki katika uzinduzi huo kuwa Uturuki ina utajiri mwingi ambao walikuwa hawautambui.

Picha za kituo hicho cha utamaduni zilioneshwa kwa uznduzi huo.

Maktaba, ukumbi wa maigizo, jumba la makumbusho na vituo vingine vingi vitajuishwa katika kituo hicho pindi ujenzi wake utakapomalizika.

AKM , jumba la utamaduni hilo linatarajiwa kumalika mwaka 2019.Habari Zinazohusiana