Rais Erdoğan katika jumba la utamaduni la Ankara

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ameshirikina na  mke wake  katika hafla ya iftar ilioandaliwa  na tawi la vijana na wanawake wa chama cha AKP katika jumba la utamaduni la Altındağ mjini Ankara

756270
Rais Erdoğan katika jumba la utamaduni la Ankara

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ameshirikina na  mke wake  katika hafla ya iftar ilioandaliwa  na tawi la vijana na wanawake wa chama cha AKP katika jumba la utamaduni la Altındağ mjini Ankara.

Watu walioshiriki katika hafla hiyo walipendezwa na kumbukumbu za rais Erdoğan.

Kabla ya hotuba ya rais Erdoğan  filamu ya tawi la wanawake na vijana katika chama cha AKP  ilitazamwa.

Rais Erdoğan katika fialamu hiyo  alizungumzia ukumbusho alioachiwa na mtoto  mdogo wa kike  ambae alimzawadia bangili.

Rais Erdoğan alizungumzia wakati alikuwa mjini Isatnbul, mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa kati ya miaka 7 au  minane alijielekeza kwa rais Erdoğan na kwamwambia kuwa alikuwa na zawadi kutoka kwa mama yake. Mtoto huyo alimpa zawadi hiyo na kumwambia kuwa imetoka kwa mama yake na kumpa ujumbe kuwa asiwasahau baada ya uchaguzi. Rais Erdoğan alisema kuwa muda wote aliokuwa katika magereza  Pınarhisar alikuwa akiona picha ya mtoto huyo ikimjia.

 Baada ya filamu hiyo kumalizika  rais Erdoğan alipongezwa huku akishindwa kujizuia kutokwa na machozi.Habari Zinazohusiana