Istanbul mji wa utamaduni

Istanbul mji wa sanaa na utamaduni

407779
Istanbul mji wa utamaduni

Istanbul ni mji ambao umepitiwa na ustaarabu wa aina mbalimbali kwa karne nyingi zilizopita. Istanbul ndio mama wa sanaa na tamaduni za aina mbalimbali. Aidha kutokana na kuwa mji mkuu wa dola nyingi huko kale, siasa ya jiji la Istanbul imeonesha kuwa na ukomavu wa aina yake.

Ukiangalia kwa undani namna utamaduni wake unavyoshabihiana, sanaa yake inavyojikamilisha pamoja na ubunifu wa kuutengeneza mji huu ni vigezo tosha vya kuupendezesha mji wa Istanbul.

Imetimia miaka 11 sasa ambapo kila mwezi September kumekua na maadhimisho ya sanaa katika jiji hili la Istanbul. Mnamo tarehe 12 September mwka 2009 ilikua ni siku ya kimataifa ya maadhimisho ya sanaa. Maadhimisho haya mwaka huu yalidumu mpaka November 8.

Kuna waandazi maarufu sana wa matamasha yote jijini Istanbul. Waandaji hawa si wengine bali ni mfuko wa Sanaa na utamaduni Istanbul ambao tangu mwaka 1987 wamejitahidi kuwaleta pamoja wasanii, na watu maarufu mbalimblali katika matamasha.

Mwaka huu pia hawakua nyuma kuandaa maadhimisho ya kimataifa ya Sanaa.

Mpaka sasa mfuko huu umeshaandaa maadhimisho 10 ya kimataifa ambayo kwa kawaida hufanyika kila baada ya miaka miwili ambapo wasanii wan je na ndani ya nchi hujumuika pamoja kuburudisha hadhira. Pia miji kama Venice, Sao Paulo na Sydney imewahi kuandaa maadhimisho haya.

Aidha maadhimisho haya sio tu yanawasaidia wasanii wa Uturuki na Sanaa yao, bali pia Sanaa ya kimataifa na wasanii wa kimataifa. Maadhimisho haya ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili hutoa fursa, mikutano na warsha mbalimbali kwa wasanii na hadhira yao ambao hupata kujifunza mambo mengi.

Maadhimisho ya kimataifa ya Biennel mwaka huu yanabeba ujumbe wa “Threepenny Opera” ambao ulikua ni ujumbe wa maigizo yaliyotungwa na Elizabeth Hauptmann na Kurt Weill mwaka 1928 na wimbo wa “insan neylle yaşar?” binadam anaishi na nini.

Kama walivyounga mkono matamasha yaliyoandaliwa na mfuko wa utamaduni na Sanaa Istanbul mwaka 2009 na 2010, wakala wa kituo cha utamani wa Ulaya Istanbul 2010 wameunga mkono uandalizi wa maadhimisho haya mwaka huu.

Kuna miradi 141 ambayo inatarajiwa kutimizwa katika matamasha haya mwaka huu huku wasanii 40 kutoka sehemu mbalimbali pamoja na makundi 70 ya wasanii yakitarajiwa kuhudhuria.

Aidha maadhimisho haya yatawakutanisha wasanii wengi maarufu duniani. Ukiachana na wasanii maarufu wa Kituruki, wasanii kama Nam June Paik, Sanja Ivekovic, Danica Dakic na RabiH Mroue watakuepo.

Soma pia: Utalii halali Uturuki


Tagi:

Habari Zinazohusiana