Mila, Imani na Utamaduni wa kituruki

Mila imani za Kituruki kuhusiana na kuabudu jua, mwezi,upinde wa mvua na radi

359295
Mila, Imani na Utamaduni wa kituruki

Kumekua na imani na mila nyingi za kuabudu mwezi, jua, upinde wa mvua, rad na mvua katika maeneo ya Mashariki ya kati hadi Anatolia.Alama na ishara nyingi zilitumiwa na watu wa Anatolia katika ibada zao mfano jua lilipewa jinsia ya kike, mwezi jinsia ya kiume, jua lilipewa heshima kama mama na mwezi kama baba. Aidha jua lilimaanisha joto, mwezi ulimaanisha baridi, jua lilimaanisha upande wa kusini huku mwezi ukiashiria kaskazini.
Leo tutaelezea heshima ya Waturuki wa zamani kwa nyota mwezi na jua na namna walivyoviingiza vitu hivi katika maisha yao ya kila siku.

katika jamii ya Waturuki kulikua na imani na mila mbalimbali kuhusiana na jua. Kulingana na vyanzo vya usimulizi wa imani za Kituruki vinasema kuwa Mungu aliuumba mwezi kuwa mwanaume na jua kama mwanamke. Akaliamrisha jua litembee mchana na mwezi utembee usiku. Hii ndiyo sababu jua lina madoadoa. Mwezi ulikua ukilicheka jua kwa madoa hayo. Na hii ndiyo sababu iliyopelekea muonekano wa mwezi kuwa kama tabasam.
Na kuhusiana na madoa juu ya uso wa mwezi, maelezo yafuatayo yalitolewa. Siku moja mwezi alienda kumtembelea jua. Alimkuta jua anakanda unga wa mikate. Basi jua alipomuona mwezi alikasirika sana akampiga kibao usoni na hivyo alama ya vidole vyake na unga ule ukabaki usoni mwa mwezi. Na hii ndiyo sababu mwezi una alama katika uso wake.

Aidha kulikua na maelezo kuhusiana na imani juu ya mwezi. Wanawake walikua wakiwapa mtihani wartoto wao wa nani atauona mwezi awali ya wengine wakati ukiwa unaandama. Hivyo watoto wakawa kila usiku wanaangalia angani ili kuona hilali mwandamo. Endapo mtoto wa kwanza kuuona mwezi atakua ni binti basi waliamini kuwa mwezi huo utakua ni wa baraka na neema kwao. Na endapo mtoto wa kiume atawahi kuona hilali mwandamo basi mwezi huo uliaminika kuwa ni wa matatizo na balaa.

Mtu huyo ambaye amebahatika kuona hilali mwandamo huaminika kuwa na bahat na baraka. Wanawake wajawazito pia walikua wakiangalia mwezi. Endapo wakiangalia mwezi alafu mtoto akacheza tumbani, mtoto huyo akiwa wa kiume basi atakua mpambanaji na jasiri na akiwa wa kike basi atakua mwenye baraka nyingi.

Pia kuna imani za asili kuhusiana na kupatwa kwa jua na mwezi. Baadhi ya imani hizo ni pamoja na kuamini kuwa kupatwa kwa mwezi na jua ni alama ya kiama. Au kuamini kuwa mtu mashuhuri amefariki. Mwaka ambao jua au mwezi umepatwa unaaminika kuwa mwaka wa matatizo na vita vyaweza kutokea.

Aidha wakati kupatwa kwa jua au mwezi kunapotokea basi matukio mengi hufanyika. Mfano, watu huchukua silaha na kupiga, husoma adhana na kusema shahada ya dini ya kiislam.
Kuhusiana na upinde wa mvua, wote waliamini kuwa upinde huunganisha mbingu na ardhi. Walikua wakiuchukulia upinde huu kama daraja maalum la Mwenyezi Mungu. Upinde ulipewa majina mbalimbali katika jamii ya Waturuki wa zamani kama vile “kirmizi yeşil” , “nur”, “al yeşil çokmesi” na kadhalika.

Na kwa upande wa radi pia waliamini kuwa sehemu ambapo radi imepiga basi ni sehemu takatifu hiyo. Ukiachana na hilo walikua wakiamini kuwa radi hii haijawaletea baraka watu na wanyama waishio sehemu hiyo. Ndio maana watu hawakupenda kulikaribia eneo lililopigawa na radi au kuwapeleka wanyama wao sehemu hiyo.
Hizi ni baadhi ya imani na mila za Waturuki wa zamani. Zinaelezea imani za Waturuki kwa jua na mwezi na baraka ambazo mwenyezi mungu ameweka kwa vitu hivi.


Tagi:

Habari Zinazohusiana