Rafael Nadal atinga fainali Barcelona Open

Rafael Nadal afanikiwa kuingia kwenye fainali za mashindano ya tenisi ya Barcelona Open ya Uhispania

1627971
Rafael Nadal atinga fainali Barcelona Open

Rafael Nadal, ambaye yuko katika nafasi ya tatu kwa wanaume katika orodha ya wanatenisi bora ulimwenguni,  alifanikiwa kuingia kwenye fainali za mashindano ya tenisi ya Barcelona Open.

Katika nusu fainali ya wanaume ya mashindano hayo ya Barcelona Open ya sakafu ya mchangani yaliyofanyika Uhispania, Nadal alikabiliana na raia mwenzake, Pablo Carreno Busta.

Baada ya kumshinda mpinzani wake katika muda wa saa 1 na dakika 29 kwa seti mbili za msururu wa 6-3 na 6-2, Nadal alijiandikisha kwenye fainali hizo kwa mara ya 12 kwenye Barcelona Open.

Nadal, ambaye ana mataji 11 kwenye mashindano hayo, atacheza mechi ya mwisho na mchezaji nambari 5 wa ulimwengu Stefanos Tsitsipas, ambaye alimshinda Mtaliano Jannik Sinner seti 2-0 za msururu wa  6-3 kwenye nusu fainali nyingine.Habari Zinazohusiana