Ubaguzi wa rangi kwenye mechi ya La Liga

Mchezaji soka wa Valencia Mouctar Diakhaby atolewa matamshi ya kibaguzi kwenye mechi ya La Liga

1614962
Ubaguzi wa rangi kwenye mechi ya La Liga

Katika mechi ya wiki ya 29 ya ligi kuu ya soka ya La Liga nchini Uhispania iliyochezwa kati ya Cadiz na Valencia, matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa dhidi ya mchezaji soka wa Ufaransa Mouctar Diakhaby yalizua utata.

Diakhaby, ambaye alidai kwamba mchezaji soka wa Uhispania Juan Torres Ruiz, anayejulikana kwa jina la utani kama "Cala" wa timu ya Cadiz, alimtolea matamshi ya kibaguzi katika dakika ya 29, wakati mechi ilipokuwa ikiendelea kwa sare ya 1-1, na kupewa kadi ya njano na mwamuzi.

Mara tu baada ya tukio hilo, timu nzima ya Valencia pamoja na benchi la ufundi walimuunga mkono Diakhaby kwa kuondoka uwanjani na kwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Katika timu ya Valencia ambayo ilirudi uwanjani baada ya dakika 15, Hugo Guillamon aliingia mchezo badala ya Diakhaby aliyekataa kuendelea na mechi hiyo.

Mechi iliendelea kuchezwa kutoka dakika ya 29 hadi mwisho.

Mchezaji wa timu ya Cadiz,  Cala ambaye anadaiwa kutoa matamshi ya kibaguzi aliendelea kubaki uwanjani hadi kipindi cha pili na kubadilishwa na mchezaji Marcos Mauro.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya La Liga, timu ilichukuwa hatua ya kujiondoa uwanjani kwa sababu ya tukio lililohusishwa na ubaguzi wa rangi kwenye soka.

Mechi hiyo kati ya Cadiz na Valencia iliisha 2-1 licha ya maneno ya kibaguzi kumfanya Diakhaby kutaka kuizuia isiendelee.Habari Zinazohusiana