Uturuki yahifadhi nafasi yake kwenye orodha ya FIBA

Timu ya kitaifa ya Uturuki ya mpira wa kikapu yahifadhi nafasi yake ya 15 kwenye orodha ya FIBA

1594412
Uturuki yahifadhi nafasi yake kwenye orodha ya FIBA

Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kimataifa la FIBA ​​limechapisha orodha ya timu bora za kitaifa za  wanaume Duniani.

Timu ya Kitaifa ya Uturuki ilihifadhi nafasi yake katika hatua ya 15.

Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kimataifa la FIBA ​​lilichapisha orodha hiyo kwa kuzingatia matokeo ya michuano ya mwisho ya mchujo ya ksuhiriki Mashindano ya Kombe la Bara Ulaya.

Kwa mujibu wa orodha hiyo; Marekani iliendelea kubaki kileleni, Uhispania ambayo ni bingwa wa mwisho wa ulimwengu ikiwa nafasi ya pili, na Australia ikashika nafasi ya tatu.

Argentina ilifuatia katika nafasi ya 4 na Serbia nafasi ya 5. Uturuki ambayo imeshinda mechi 3 za mwisho katika michuano ya mchujo na kufuzu Mashindano ya Ulaya ya mwaka 2022, ilihifadhi nafasi yake.

Uturuki ambayo imefanikiwa kufuzu mashindano ya Ulaya kwa mara ya 14 mfululizo, inalenga kujinyakulia tiketi ya kushiriki mashindano ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020.

Timu ya kitaifa itashiriki kwenye mechi za mchujo za kutafuta nafasi kwenye michezo ya Olimpiki huko Victoria, Canada kuanzia tarehe 29 Juni hadi 4 Julai.Habari Zinazohusiana