Barcelona yatinga fainali Copa del Rey

Barcelona yaishinda Sevilla 3-0 kwenye mechi marudiano ya nusu fainali ya Copa del Rey

1595154
Barcelona yatinga fainali Copa del Rey

Barcelona ilikuwa timu ya kwanza kuingia fainali ya kombe la Copa del Rey nchini Uhispania baada ya kuishinda Sevilla 3-0 katika mechi ya marudiano ya nusu fainali.

Timu hiyo ya Catalonia ambayo ilishindwa 2-0 na Sevilla ugenini kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali, ilipindua matokeo hayo katika mechi ya marudiano kwa kufunga mabao 3.

Kipindi cha kwanza cha mechi kilimalizika wakati Barcelona inaongoza 1-0 kupitia bao lililofungwa na Ousmane Dembele dakika ya 12.

Baada ya muda wa kawaida wa mechi, Brcelona ilipata bao katika dakika za mwisho za ziada (Dak. 90 + 4) kupitia Gerard Pique na mechi ikaisha 2-0  na kulazimika kuchezwa muda wa nyongeza.

Mwanzoni mwa muda wa nyongeza, Martin Braithwaite alifunga bao katika dakika 95 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jordi Alba na kumalizika 3-0.

Barcelona ambayo imeshinda Kombe la Copa del Rey mara 30 na kuwa timu iliyocheza fainali nyingi zaidi (mara 41), na imeweza kucheza katika fainali mara ya 9 katika misimu 10 ya mwisho.

Katika nusu fainali nyingine ya Kombe hilo, Levante na Athletic Bilbao zitacheza usiku wa leo saa 23:00. Mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Bilbao ilimalizika 1-1.Habari Zinazohusiana