Alex amshinda Hagi kwa kura za FIFA

Mchezaji wa zamani wa Fenerbahçe apata kura nyingi zaidi kuliko mchezaji wa zamani wa Galatasaray Hagi

1594380
Alex amshinda Hagi kwa kura za FIFA

Katika upigaji kura wa SPORTS FIFA, Alex amempita Hagi.

Shirikisho la Soka Ulimwenguni la FIFA liliandaa mchakato wa upigaji kura kuhusu "Nani alikuwa mchezaji bora?" kati ya Alex de Souza na Gheorghe Hagi.

Upigaji kura ulioanzishwa na FIFA.com kulinganisha mchezaji soka wa zamani wa Romania Hagi aliyekuwa nambari 10 maarufu wa Galatasaray, na Alex wa Brazil aliyevaa nambari 10 ya jezi ya Fenerbahçe.

Takriban mashabiki elfu 515 wa soka walishiriki mchakato huo ambapo Alex alimpiku Hagi kwa kukusanya jumla ya asilimia 50.4 ya kura.

Hagi, ambaye alichezea Galatasaray kuanzia mwaka 1996 hadi kustaafu kwake mwaka 2001, alicheza jumla ya mechi 192 kwenye timu ya Galatasaray.

Alex naye alivaa jezi ya Fenerbahçe na kuichezea mechi 344 kati ya mwaka 2004-2012.Habari Zinazohusiana