Lakers yaishinda Warriors 117-91 kwenye NBA

Mabingwa watetezi Los Angeles Lakers wapata ushindi dhidi ya Golden State Warriors kwenye NBA

1592633
Lakers yaishinda Warriors 117-91 kwenye NBA

Timu ya Los Angeles Lakers ambayo ndio bingwa wa mwisho wa Ligi ya mpira wa kikapu ya NBA nchini Marekani, ilipambana na Golden State Warriors usiku wa jana.

Ligi ya NBA iliendelea na mechi 7 zilizochezwa hapo jana.

Los Angeles Lakers ilifanikiwa kuondoka na ushindi muhimu baada ya kuipiga Golden State Warriors 117-91 kwenye mechi hiyo.

Baada ya kupoteza michezo nne mfululizo, Lakers ilianza kwa kasi kubwa mechi hiyo na kuongoza 41-21. Mabingwa watetezi wa Los Angeles walionyesha umahiri wao katika uwanja wao wa Staples Center na kumaliza kwa ushindi 117-91 dhidi ya Golden State Warriors.

Matokeo kamili ya mechi zote zilizochezwa usiku wa jana ni kama ifuatavyo:

Boston Celtics-Washington Wizards: 111-110

Houston Rockets-Memphis Grizzlies: 84-133

Miami Heat-Atlanta Hawks: 109-99

Detroit Pistons-New York Knicks: 90-109

Los Angeles Lakers-Golden State Warriors: 117-91

Minnesota Timberwolves-Phoenix Suns: 99-118

Sacramento Kings-Charlotte Hornets: 126-127Habari Zinazohusiana