Nadal na Medvedev watinga robo fainali Australia Open

Rafael Nadal na Daniil Medvedev wafanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Australia Open

1583933
Nadal na Medvedev watinga robo fainali Australia Open

Mhispania Rafael Nadal na Mrusi Daniil Medvedev walifanikiwa kuingia robo fainali kwenye michuano ya Australia Open ambayo pia ni mashindano ya kwanza makubwa ya msimu wa tenisi.

Siku ya 8 ya mashindano hayo yanayoendelea mjini Melbourne ilianza na mechi zilizochezwa nyakati za asubuhi.

Kwa upande wa wanaume, mchezaji nambari 2 kutoka Uhispania Rafael Nadal alimshinda mchezaji nambari 16 kutoka Italia Fabio Fognini seti 3-0 za msururu wa 6-3, 6-4 na 6-2 katika raundi ya nne na kuingia robo fainali.

Katika harakati za kufukuzia taji kubwa la 21 la tenisi, Nadal atachuana na mshindi wa mechi kati ya Stefanos Tsitsipas na Matteo Berrettini katika robo fainali.

Kwingineko, Danieli Medvedev wa Urusi ambaye ni mchezaji nambari 4 alimshinda Mackenzie McDonald wa Marekani seti 3-0 za msururu wa 6-4, 6-2 na 6-3.

Medvedev atachuana na raia mwenzake ambaye ni mchezaji nambari 7 Andrey Rublev katika robo fainali.

Kwa upande wa wanawake, Mmarekani Jessica Pegula, ambaye anashika nafasi ya 61 ulimwengu alishangaza wengi kwa kumshinda mchezaji nambari 5 wa Ukraine Elina Svitolina seti 2-1 za msururu wa 6-4, 3-6 na 6-3 na kuingia robo fainali.

Pegula atakabiliana na raia mwenzake nambari 22 Jennifer Brady katika robo fainali.Habari Zinazohusiana