Spurs wawashinda Lakers kwenye NBA
Mabingwa watetezi wa NBA Los Angeles Lakers washindwa na San Antonio Spurs kwenye NBA
Timu ya Los Angeles Lakers ilishindwa 118-109 na timu ya San Antonio Spurs kwenye mechi ya ligi ya mpira wa kikapu ya NBA nchini Marekani.
Ligi hiyo ya NBA iliendelea na mechi 5 zilizochezwa usiku wa jana.
San Antonio Spurs ilifanikiwa kuishinda Los Angeles Lakers ambao ndio mabingwa wa mwisho wa NBA, waliokuwa wameshinda mechi 4 mfululizo.
Katika timu ya Spurs, LaMarcus Aldridge ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa timu hiyo aliyemaliza mechi na pointi 28, huku DeMar DeRozan akichangia pointi 19 na Dejounte Murray pointi 18.
LeBron James wa Lakers naye alimaliza mechi na pointi 27, asist 12, rebound 6, huku Anthony Davis akimaliza na pointi 23, asist 3 na rebound 10.
Kwingineko Cleveland Cavaliers iliwashinda Memphis Grizzlies 94-90 kwenye mechi ambayo mchezaji wa timu ya taifa Cedi Osman alimaliza na pointi 16, asist 7 na rebound 5.
Andre Drummond wa Cavaliers alimaliza na "double-double" za pointi 22 na rebound 15, huku Larry Nance akichangia pointi 18.
Mchezaji wa Grizzlies Jonas Valanciunas, alimaliza na pointi 17 huku Brandon Clarke akichangia pointi 14 ambazo hazikuweza kuwapa ushindi.
Matokeo kamili ya mechi zote zilizochezwa hapo jana ni kama ifuatavyo;
Brooklyn Nets-Philadelphia 76ers: 122-109
Memphis Grizzlies-Cleveland Cavaliers: 90-94
Portland Trail Blazers-Minnesota Timberwolves: 135-117
Denver Nuggets-Dallas Mavericks: 117-124
Los Angeles Lakers-San Antonio Spurs: 109-118
Habari Zinazohusiana

Mechi za kufuzu Kombe la Dunia zaahirishwa Amerika ya Kusini
CONMEBOL yaahirisha mechi za kufuzu Kombe la Dunia la 2022 za Amerika ya Kusini kutokana na Covid-19
Ushindi wa Juventus dhidi ya Lazio Serie A
Juventus yaishinda Lazio 3-1 kwenye mechi ya ligi kuu ya soka ya Serie A nchini Italia