Msaada kutoka kwa Mesut Özil

Nyota wa kabumbu wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki  atoa msaada  kwa familia  280 Manisa Uturuki

1418990
Msaada kutoka kwa Mesut Özil


Nyota wa kabumbu wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki  atoa msaada  kwa familia  280 Manisa Uturuki.

Mesut Özil, nyota wa kabumbu katika timu ya taifa ya Ujerumani na timu ya Arsenal nchini Uingereza ametoa msaada kwa familia  280 Manisa nchini Uturuki.

Msaada huo umetolewa kwa shirika la misaada la Uturuki  la Kızılay  na kukabidhiwa kwa  walengwa wanaohitaji msaada nchini Uturuki.

Özil amesema kwamba , msaada huo ni  katika zoezi la kuunga mkono  kampeni  ilioanzishwa na Kızılay  kwa kauli mbiu "Itakwisha iwapo tutashirikiana".

Msaada huo wa chakula  umetolewa kwa familia  280  katika kitongoji cha Soma na Yunusemre  mjini Manisa kwa walengwa.

Mkurugenzi wa  shirika la Kızılay Manisa, Serdar Sevim ametoa shukrani kwa Mesut Özil kwa msaada wake huo ambao unastahili pongezi.
 Habari Zinazohusiana