Shirika la kabumbu la Uingereza  lafuta mechi zote hadi Mei

Shirika la soka la Uingereza limetangaza kuahirisha  mechi zote  hadi

1381501
Shirika la kabumbu la Uingereza  lafuta mechi zote hadi Mei


Shirika la soka la Uingereza limetangaza kuahirisha  mechi zote  hadi kutakapotangazwa upya ifikapo Mei.

Shirika la soka la Uingereza  limetangaza kuahirisha michuano yote ya kabumbu ya ligi kuu ya Uingireza  kutokana na virusi vya corona aina ya Covid-19.

Shirika hilo la soka la Uingereza limefahamisha kuwa mechi zote zimeahirishwa hadi  iifikapo mwezi Mei bila ya tarehe kamili kutolewa.

Michuano ya  Ligi  daraja la kwanza nchini Uingereza  na Super League  ya wanawake zimeahirishwa hadi  mwezi ujao kwa lengo la kupunguza  na kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya corona.

Taarifa pia iliotolewa na shirika la  soka la Ulaya UEFA  imefahamisha kuahirisha michuano yote  ya kabumbu  ya mwaka  2020.

Uamuzi uliochukuliwa  na shirika la soka la Uingereza  umepongezwa na UEFA.


Tagi: #corona , #UEFA

Habari Zinazohusiana