Mashindano ya soka ya mataifa ya Ulaya (EURO 2020) yahairishwa

Mashindano ya mataifa ya Ulaya ya 2020 (Euro 2020 ) yaahirishwa kwa mwaka mmoja

1379923
Mashindano ya soka ya mataifa ya Ulaya (EURO 2020) yahairishwa

Mashindano ya mataifa ya Ulaya ya 2020 (Euro 2020 ) yaahirishwa kwa mwaka mmoja.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka la Norway kupitia ukurasa wao Twitter ilisema kwamba mashindano ya soka ya UEFA 2020 yameahirishwa kwa mwaka mmoja na yatafanyika kati ya Juni 11 na Julai 11, 2021.

Kufuatia tishio la virusi vipya vya Corona,nchi wanachama wa UEFA walifanya mkutano kwa njia ya teleconferanse na kufikia uamuzi wa kuhairisha mashindano kwa mwaka mmoja.

Kuhusiana na ligi ya vilabu na ligi ya klabu bingwa za UEFA, masuala hayo yatajaliwa katika mkutano ujao. Hata hivyo mashindano hayo 2 yameahirishwa kwa muda.

Ni lini mashindano hayo yatarejea tena itategemeana hali ya mlipuko itakavyokuwa.Habari Zinazohusiana