Kinda la miaka 17 lang'ara Barcelona ikiibuka kifua mbele

Anssumane Fati aitoa kimasomaso Barcelona na kuipa ushindi zidi ya Levante.

Kinda la miaka 17 lang'ara Barcelona ikiibuka kifua mbele
2020_Subat_fati_2.jpg
2020_Subat_fati_1 (1).jpg

Katika wiki ya 22 ya ligi kuu ya Uhispania (La Liga), Barcelona imefanikiwa kuichapa Levante goli 2-1.

Magoli ya Barcelona yalipatikana kipindi cha kwanza kupitia nyota anayeibukia kinda la miaka 17, Forveti Anssumane Fati ( Dk 30 na Dk. 32)

Magoli yote mawili ya Fati, aliyafunga baada ya kumalizia pasi kutoka kwa mkali Lionel Messi.

Fati amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga goli kwenye mashaindano ya La Liga.

 Habari Zinazohusiana