Sadio Mane atwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika

Tuzo ya CAF ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2019 imeenda kwa winga machachari raia wa Senegal, Sadio Mane

Sadio Mane atwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika

Sadio Mane winga machachari raia wa Senegal anayekiputa  Liverpool timu inayopatikana mitaa ya London kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2019 wa Afrika.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) imesema tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika imempata mwenyewe katika hafla iliyofanyika katika mji wa Hurgada nchini Misri.

Tuzo hiyo pia ilikuwa ikiwaniwa na Muhammed Sallah wa Misri na Riyad Mahrez wa Algeria.

Mane (27) alikuwa namchango mkubwa msimu uliopita kuiwezesha Liverpool kutwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya, hali kadhalika aliiwezesha timu yake ya taifa ya Senegal kumaliza nafasi ya pili katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika.Habari Zinazohusiana