Manchester City watakata dhidi ya Everton

Manchester City yatakata wakiikaribisha Evarton katika dimba la Etihad

Manchester City watakata dhidi ya Everton

Wiki ya 21 ya ligi kuu ya Uingereza ilitimua vumbi katika viwanja mbalimbali. Manchester City walifanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Evarton. City ambao ni mabingwa mara 2 mfululizo hivi karibuni walikuwa wenyeji wa mchezo huo katika dimba lao la Etihad.

City walipata magoli yao mnamo dk 51 na 58 kupitia kwa Gabriel Jesus, huku Everton wakipata goli la kufutia machozi kupitia Richarlison dk 71.

Kwa matokeo hayo Manchester City wanafikisha alama 44 na Everton wanabaki na alama 25.

Matokeo mengine ni kama ifuatavyo,

Brighton & Hove Albion-Chelsea: 1-1

Burnley-Aston Villa: 1-2

Southampton-Tottenham: 1-0

Newcastle United-Leicester City: 0-3

Watford-Wolverhampton: 2-1

West Ham United-Bournemouth: 4-0

Norwich City-Crystal Palace: 1-1

Manchester City-Everton: 2-1

 

 Habari Zinazohusiana