Wanamieleka mtindo wa "Grecoroman" wajizolea medali huko Urusi

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uturuki ya mieleka mtindo wa Grecoroman wajizolea medali huko Urusi

Wanamieleka mtindo wa "Grecoroman" wajizolea medali huko Urusi

Timu ya taifa ya Uturuki ya mieleka mtindo wa “Grekoroman” imenyakua medali 3 za fedha na 1 ya shaba katika mashindano ya Grand Prix Moscow Alrosa.

Baraza la mieleka la Uturuki limetoa taarifa kwamba wachezaji 4 wa timu ya taifa wameibuka kidedea na kufanikiwa kunyakua medali katika mashindano yaliyofanyika mjini Moscow.

Katika mashindano hayo Atakan Yüksel, kilo 67, Meteheani Başarkilo 87 na kwa upande wa kilo 97 Ibrahim Tığcı walifanikiwa kutwaa medali za fedha huku Yunus Emre Başar akitwaa medali ya shaba upande wa kilo 77.Habari Zinazohusiana