Si Valencia wala Chelsea...

Wiki ya 5 ya mashindano ya ligi ya mabingwa UEFA imezikutanisha timu za kundi H za Chelsea na Valencia

Si Valencia wala Chelsea...
Kepa Arrizabalaga.JPG
Valencia Francis Coquelin   Chelsea Michy Batshuayi.JPG
Valencia Lee Kang    Chelsea N'Golo Kante.JPG
Valencia v Chelsea.JPG
Valencia Rodrigo Moreno    Chelsea Kurt Zouma.JPG

Wiki ya tano ya mashindano ya ligi ya mabingwa ya UEFA imeendelea. Katika kundi H, Chelsea ilikaribishwa na Valencia.

Dk 40 ya mchezo Soler aliipatia Valencia goli la kuongoza, ambalo halikudumu muda mrefu kwani dk 1 baadaye Chelsea walisawazisha kupitia mchezaji wao Kovacic.

Katika kipindi cha pili Chelsea waliuanza mchezo kwa kasi na Dk ya 50 walipata goli la 2.

Wenyeji Valencia mnamo dk 82 kupitia kwa Daniel Wass walisawazisha goli, na mpaka mwisho wa mchezo ubao wa matokeo ulisomeka 2-2.

Kwa matokeo hayo timu zote hizo mbili za kundi H zimefikisha alama 8.Habari Zinazohusiana