Messi wa maajabu aibeba Barcelona

Apachika 2 katika ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Manchester, na kuibebeba Barcelona hadi nusu fainali UEFA

00016366801.jpg

Barcelona imefanikiwa kuichapa Manchester United goli 3-0 katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya.

Barcelona ambayo mchezo wa kwanza ilishinda kwa goli 1-0. Imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali. Mashetani wekundu kama inavyojulikana Manchester Unt waliuanza mchezo huo kwa kasi. Ikiwa ni dakika za mwanzo tu Rashford akiwa amebaki na kipa alipiga shuti ambalo liligonga mwamba.

Barcelona ikiongozwa na Messi baadae iliutawala mchezo. Messi aliandika goli la kwanza dk ya 16, dakika 4 baadae mnamo dk ya 20 kutokana na makosa ya mlinda mlango wa Man U, De Gea, Messi alipachika goli la 2. Goli la 3 katika mchezo huo lilipatikana kipindi cha pili dk ya 61 kupitia kwa Coutinho.Habari Zinazohusiana