Ajax yafanya maajabu kwa mara nyingine

Yafanikiwa kutinga nusu fainali kwa ushindi wa goli 2-1 shidhi ya Juventus, hii ni baada ya kuifungashia virago Real Madrid hatua ya 16 bora

800x800.jpg
00016367626.jpg
00016366729.jpg
00016366723.jpg
00016366598.jpg

Ajax yafanikiwa kutinga nusu fainali za kombe la klabu bingwa Ulaya (UEFA).

Ajax ambayo ni timu yenye wachezaji wachanga, ilifanikiwa kuitoa Real Madrid katika hatua ya 16 bora na hivyo kutinga robo fainali.Katika michezo ya robo fainali ilikutana na Juventus.  Ambapo mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1.

 Katika mchezo wa marudio uliochezwa Turin Juventus wakiikaribisha Ajax, ulimalizika kwa Ajax kupata ushindi wa goli 2-1.

Goli la Juventus lilipatikana dk 28 kupitia kwa Cristiano Ronaldo. Kwa upande wa Ajax magoli yaliyowaletea ushindi yalipatikana dk 34 kupitia kwa  Donny van na dk ya 67 kupitia kwa Matthijs ligt.

Kwa matokeo hayo Ajax imefanya maajabu kwa mara nyingine kwa kuwatoa miamba wa soka Juventus na Real Madrid na hivyo kufanikiwa kutinga nusu fainali.Habari Zinazohusiana