Timu ya taifa ya soka ya Burundi yawapa raha Warundi kwa kutinga fainali za AFCON

Yafuta ndoto za Gabon katika siku ya kihistoria mjini Bujumbura kwa kufuzu kwa mara ya kwanza kutinga fainali za AFCON

Timu ya taifa ya soka ya Burundi yawapa raha Warundi kwa kutinga fainali za AFCON

Cedric Amissi, alifunga goli dk ya 76 lililoipa matumaini makubwa Burundi ambayo ilikuwa ikihitaji sare katika mchezo huo  dhidi ya Gabon kuweza kusonga mbele katika fainali zitakazochezwa Misri.

Dk 8 kabla mchezo kumalizika Omar Ngando aliipa wakati mgumu Burundi baada ya kujifunga, kitu kilichoipa nguvu Gabon kutafuta ushindi waliokuwa wakiuhitaji kuweza kufudhu fainali hizo.

Gabon pamoja na kumcheza mshambuliaji wao nyota anayechezea Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, hawakufua dafu mbele ya Burundi, ambao walikuwa mbele ya mashabiki zao katika siku nzuri kabisa kwa Warundi mjini Bujumbura.

Kwa matokeo hayo Burundi iliyomaliza nafasi ya pili kundi C nyuma ya Mali  imekata tiketi ya fainali za AFCON. Huku Gabon ambao ndio walikuwa waandaaji wa fainali hizo 2017 wakitupwa nje ya michuano  kwa kumaliza nafasi ya tatu.

Burundi -  ambayo inashika nafasi ya 138 katika orodha ya timu bora za Fifa itaungana na majirani zao wengine Kenya na Uganda ambazo nazo zimeshafuzu kucheza fainali hizo za AFCON 2019 .

AFCON  2019  kwa mara ya kwanza itaanza kutimua vumbi mwezi Juni na Julai na itajumjuisha timu 24 badala ya 16.

 Habari Zinazohusiana