Tarehe ya kihistroria katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya

Mfumo mpya wa kumsaidia mwamuzi, VAR, watumika kufuta goli lililolalamikiwa, Benzema na Ramos nao waweka rekodi

2019-02-13T215909Z_69931384_RC1C03B9AA20_RTRMADP_3_SOCCER-CHAMPIONS-TOT-DOR.JPG
2019-02-13T214808Z_1162909921_RC13DC7249B0_RTRMADP_3_SOCCER-CHAMPIONS-TOT-DOR.JPG
2019-02-13T211542Z_295688784_RC1ADDD2B3E0_RTRMADP_3_SOCCER-CHAMPIONS-TOT-DOR.JPG
2019-02-13T204322Z_1171347952_RC1985F30F20_RTRMADP_3_SOCCER-CHAMPIONS-AJA-MAD.JPG
2019-02-13T212441Z_390224037_RC197F3A6410_RTRMADP_3_SOCCER-CHAMPIONS-AJA-MAD.JPG

 

Ligi kuu ya klabu bingwa Ulaya imeendelea. Real Madrid wakikutana na Ajax, huku Tottenham wakikichapa na Borussia Dortmund.

Kwa mara ya kwanza katika mchezo kati ya Real Madrid na Ajax umetumika mfumo wa video wa kumsaidia mwamuzi "Video Asistance Refaree, VAR". Goli la la Ajax lililofungwa na Nicolas Tagliafico  dk 37 lilifutwa baada kuonekana katika mfumo huo wa VAR kuwa alikuwa ameotea. Hii ni mara ya kwanza katika historia goli linafutwa kutokana na ushahidi wa mfumo wa VAR.

Real Madrid walifanikiwa kushinda mtanange huo kwa ushindi wa goli 2-1. Mogoli ya Madrid yalipatikana dk 60 kupitia kwa Karim Benzema na dk 87 kupitia kwa Marco Asensio. Huku goli la Ajax ambao ndio walikuwa wenyeji wa mtanange huo likipatikana dk ya 75 kupitia kwa Hakim Ziyech.

Sergio Ramos kapteni wa Real Madrid alicheza mchezo wake wa 600 akiwa na timu hio.Huku Benzema akifunga goli lake la 60 katika mchezo wa ligi klabu bingwa barani Ulaya. 

Katika Uwanja wa Wimbley nako Tottenham walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund.

Magoli hayo ya Tottenham yalipatikana dk 47 kupitia kwa Son Heung-Min, dk 83 kupitia kwa Jan Vertonghen na dk 86 kupitia kwa Fernando Llorente.

 

    Habari Zinazohusiana