Luka Modriç awamaliza, Messi, Ronaldo; atwaa Ballon d'Or

Luka Modriç awamaliza, Messi, Ronaldo; atwaa Ballon d'Or

Luka Modriç awamaliza, Messi, Ronaldo; atwaa Ballon d'Or

Hatimaye mchezo wa Messi na Ronaldo kupokezana kijiti cha tuzo bora kabisa ya mwanasoka ya Ballon D'Or ambapo kila mmoja amechukua mara 5, umeisha leo baada ya Luka Modriç kutwaa tuzo hiyo. 


Messi na Ronaldo wamekua tishio katika ulimwengu wa soka na kujikuta wakitawala muongo mzima uliopita kwa kuitwaa taji hilo wao peke yao.


Lakini nyota machacha wa timu ya taifa ya Croatia na Real Madrid, Luka Modriç hatimaye ametawazwa taji hilo. 


Modriç aliisaidia timu yake ya taifa kutinga fainali za kombe la dunia mwaka huu, huku akiibeba Madrid mgongoni kutwaa taji la tatu mfululizo la klabu bingwa barani Ulaya. 


Modriç amemaliza katika nafasi ya kwanza, huku Christiano Ronaldo akitajwa kuwa ni mshindi wa pili akifuatiwa na Anthoine Griezmann aliyeisaidia Ufaransa kutwaa kombe la dunia. 


Nafasi ya nne ilikwenda beki hatari wa Ufaransa, Rafael Varane.
Lionel Messi ameshika nafasi ya tano, mara ya kwanza kwake kuwa nje ya tatu bora kwa miaka 11 iliyopita. 


Modriç yeye anatwaa taji hilo baada ya kutwaa mchezaji bora wa UEFA na mchezaji bora wa mashindano ya kombe la dunia


Tagi: Ronaldo , Messi

Habari Zinazohusiana