Arjen Robben kuachana na Bayern Munich

Arjen Robben ajiandaa kuiga Bayern Munich, ametangaza kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu

Arjen Robben kuachana na Bayern Munich

Arjen Rubben, anajiandaa kufungua ukarasa mpya katika maisha yake ya soka la kulipwa.

Robben mwenye miaka 34 kutokea Uholanzi ambaye kwa miaka 10 amekuwa akiichezea Bayern Munich,  timu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga, ametangaza mwishoni mwa msimu ataachana na timu hiyo.

Robben alisema amefurahia sana muda wote alioishi Munich, Alisema kila kitu kiko sawa kabisa lakini inabdi tu aachane na klabu hiyo.

Akiongelea kuhusu hali ya Bayern Munich kwenye ligi alisema timu inapokuwa na alama 9 nyuma ya vinara wa ligi inakuwa si tena miongoni mwa inayotazamiwa kuchukua ubingwa.

Robben alijiunga na Bayern mnamo mwaka 2009, amecheza mechi 198 na timu hiyo na kuifungia magoli 98.

 Habari Zinazohusiana