Manchester City shangwe,Man U yabanwa

Manchester City shangwe,Man U yabanwa

Manchester City shangwe,Man U yabanwa


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, Manchester City wameendeleza ubabe wa kukusanya alama 3 baada ya kuichabanga Bournamouth goli 3 kwa 1.
Magoli kutoka kwa Raheem Sterling, Bernaldo Silva na Ilkay Gündogan yalitosha kabisa kupeleka ushindi huo muhimu kwa magwiji hao. 
Wakati Man city wakingaa, mahasimu wao na majirani wao katika mji, Manchester United, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Southampton. 
Manchester walianza kuchechemea baada ya kukubali magoli mawili katika kipindi cha kwanza. 
Matokeo hayo yanaifanya Manchester United iendelee kudidimia katika msimamo wa ligi hiyo huku Manchester City ikiendelea kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo.Habari Zinazohusiana