Liverpool kileleni, Man City yachechemea

Mbio za kuusaka ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza zimeendelea Leo ambapo vilabu kadhaa vilijikita uwanjani kuwania alama 3 muhim.

Liverpool kileleni, Man City yachechemea

Mbio za kuusaka ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza zimeendelea Leo ambapo vilabu kadhaa vilijikita uwanjani kuwania alama 3 muhim. 

Liverpool walikua kibaruani kuikabili timu ya soka ya Brighton ambayo iliitoa jasho Manchester United wikiendi iliyopita. 

Goli la pekee la nyota wa Misri, Mohammed Salah liliihakikishia Liverpool ushindi na kutwaa alama tatu katika Mchezo huo wa kukata na shoka. 

Brighton walionesha uwezo mkubwa wa kuhimili vishindo vya Safi hatari ya ushambulizi ya klabu ya Liverpool inayoongozwa na Salah, Sadio Mane na Mbrazil Robert Firmino.

Wakati the Reds wakitwaa alama hizo tatu,mahasimu wao Manchester City walijikuta wakibanwa mbavu na kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Wolves. 

Tofauti na mategemeo ya wengi kwamba Wolves wangeweza kuwa chambo kwa Man city, the blues walijikuta wakichechemea Mbele ya wakali hao. 

Goli la mapema la Wolves liliwasha cheche Man city ambao walijikwamua na kusawazisha mnamo dakika ya 69 ya mchezo. 

Kwa matokeo haya, Liverpool inajikita kileleni ikiwa na alama zote 9 katika michezo yake 3, rekodi bora kabisa ya kuanzia kwa takriban misimu mitano iliyopita. Manchester City wao wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 7, baada ya kugawana alama moja moja na Wolves.Habari Zinazohusiana