Man City yapeta, Man U, Arsenal zabanwa mbavu

Man City yapeta, Man U, Arsenal zabanwa mbavu

Man City yapeta, Man U, Arsenal zabanwa mbavu

Ligi kuu ya soka nchini Uingereza imeendelea tena wikiendi hii ambapo vilabu mbalimbali vilishuka dimbani kutoana jasho. 


Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City wameendeleza ubabe katika ligi hiyo baada ya kuicharaza timu ya soka ya Huddlesfield kwa magoli 6 kwa 1.


Jahazi la Huddlesfield lilionekana kuzama mapema baada ya kukubali jumla ya magoli 4 kwa majo katika kipindi cha kwanza. Aguero alikua ni moto wa kuotea mbali katika mchezo huo, ambapo alifanikiwa kuibuka na hatrick. 


Wakati hayo yakiendelea, Vijana Wa Jose Mourinho,Manchester United walijikuta wakikalia kuti kavu na kulazimishwa kipigo cha magoli 3 kwa 2. Timu ya Soka ya Brighton iliwashangaza wengi baada ya kuwatangulia mashetani hao wekundu na kuwatundika magoli mawili kipindi cha kwanza. 
Licha ya Lukaku kujaribu kupunguza msumari mmoja, Man U walijikuta wakichabangwa goli is tatu kwa mkwaju wa Penalti. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Man U 2 Brighton 3. 


Jahazi la Arsenal limeendelea kuzama na kupoteza matumaini baada ya wiki hii pia kukubali kichapo kingine cha magoli 3 kwa 2 dhidi ya Chelsea. Hii ni mechi ya pili ya ligi hiyo msimu huu na Arsenal wameshapoteza mechi zote baada ya kukubali kipigo katika mechi ya awali dhidi ya Manchester city.


Kocha mkuu wa timu hiyo, Unai Emery anajikuta katika wakati mgumu kuwanoa washika mitutu hao kwani mashabiki wake wana uchu na ari ya kutwaa taji msimu huuHabari Zinazohusiana