Rais Erdoğan ampongeza rais wa Croatia kwa timu yake kuingia katika fainali ya kombe la dunia

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ampongeza rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarović kwa timu yake ya taifa kuingia katika fainali ya kombe la dunia nchini Urusi

Rais Erdoğan ampongeza rais wa Croatia  kwa timu yake kuingia katika fainali ya kombe la dunia

Rais wa Uturuki amempongeza rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarović kwa ushindi wa timu yake ya kabumbu ya taifa dhidi ya Uingereza na kuingia katika fainali ya kombe la dunia nchini Urusi.

Rais Erdoğan amempongeza Kolinda Grabar-Kitarović Alkhamis baada ya timu ya Croatia kuichapa timu ya Uingereza kwa mabao wawili kwa moja na kujipatia tikiti yake ya kuingia fainali.

Fainali ya kombe la dunia itachezwa kati ya Ufaransa na Croatia Jumapili na kuoneshwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha Uturuki TRT 1  Jumapili.

Rais Erdoğan alikutana na rais wa Croatia katika mkutano wa NATO mjini Brussel wakati wa mazungumzo kuhusu amani nchini Afghansitani.

Kwa upande wake rais wa Croatia amempongeza rais Erdoğan kwa ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Uturuki Juni 24.

 Habari Zinazohusiana