Mesut Özil kuachana na timu ya Ujerumani

Mchezaji maarufu wa soka Mesut Özil ametangaza kuacha kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani

Mesut Özil kuachana na timu ya Ujerumani

Mchezaji nyota wa soka Mesut Özil ametangaza kuacha kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani.

Hii ni baada ya Özil kupiga picha na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan mnamo mwezi Mei.

Picha ya pamoja ya Özil na Erdoğan ilileta kizaazaa nchini Ujerumani ambapo  mchezaji huyo alipata kashfa nyingi kutoka kwa watu tofauti  kutokana na tofauti za kisiasa.

Özil amekuwa katika wakati mgumu hasa baada ya timu ya Ujerumani kuondolewa katika kombe la dunia 2018.

Siku chache zilizopita baba yake Özil alisema kuwa "Ingekuwa ni mimi ningekuwa nimeshaachana na timu ya Ujerumani."

Kauli ya baba wa mchezaji huyo ilizua hisia nyingi nchini Ujerumani.

 Habari Zinazohusiana