Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 03.06.2021

1650723
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Yeni Şafak: "Ujumbe kwa Israeli katika MGK"

Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Kitaifa (MGK) uliofanyika jana chini ya uenyekiti wa Rais Recep Tayyip Erdoğan, Israeli ilikemewa kwa mauaji ya huko Gaza mwezi uliopita. Taarifa hiyo ilisema, "Ili kutorudia uhalifu wa kivita wa Israeli na kupata suluhisho la haki, la kudumu na la kina kwa suala la Palestina, jamii ya kimataifa inaombwa kutekeleza jukumu lake bila kuchelewa."

 

Hürriyet: "Taarifa ya Israeli kutoka kwa Waziri Çavuşoğlu"

Waziri wa Mambo ya nje Mevlüt Çavuşoğlu alisema katika taarifa yake hapo jana kwamba 'Israeli inahitaji kuachana na sera mbaya ili kudumisha uhusiano mzuri nasi.'.

 

Star: "Waziri Dönmez: Waliwekeza Euro bilioni 25 katika sekta ya nishati ya Uturuki"

Waziri wa Nishati na Maliasili Fatih Dönmez alisema kuwa pamoja na washirika wa kampuni za nishati za Ujerumani, Uturuki imewekeza takriban Euro bilioni 25 katika sekta ya nishati kwa miaka 18 iliyopita na imetoa zaidi ya ajira elfu 15, na kusema, "Takwimu hizi zinaonyesha hisa za kampuni na wawekezaji wa Ujerumani kwa sekta hiyo na ujasiri wa uchumi wa Uturuki.'

 

Haber Türk: "Takwimu za mauzo ya nje ya mwezi Mei zatangazwa"

Katika taarifa yake ya jana, Waziri wa Biashara Mehmet Muş alisema kuwa mauzo ya nje ya Uturuki ya mwezi Mei yaliongezeka kwa asilimia 65.5 ikilinganishwa na mwezi huo huo wa mwaka uliopita na yalifikia dola bilioni 16.5 na akasema, "Kwa thamani hii, tulifikia mauzo ya pili ya juu zaidi ya mwezi Mei kwa miaka yote. "

 

Sabah: "Ulimwengu unazungumzia miujiza ya SİHA za Kituruki (Vyombo vya  Anga visivyo na rubani)"

Teknolojia ya Uturuki ya vyombo vya Anga vya İHA/SİHA, ambayo imekuwa chapa ya ulimwengu katika uwanja wa jeshi, imechunguzwa na Uswizi. Katika uchambuzi ulioandikwa na huduma ya kitaifa ya utangazaji nchini, ilisisitizwa kuwa teknolojia ya Uturuki, ambayo imepokea sifa kote ulimwenguni kutokana na İHA /SİHA na imepata ushindi mwingi katika maeneo mengi haswa huko Azerbaijan na Libya, inaelezewa kama muujiza na Mataifa ya Magharibi.Habari Zinazohusiana