Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 02.06.2021

1649976
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Hürriyet: "Erdoğan: Nitamuuliza Biden kwanini wana mvutano"

Rais Recep Tayyip Erdoğan alisema kwenye mahojiano ya moja kwa moja ya Shirika la Redio na Televisheni la Uturuki (TRT) hapo jana kwamba atamuuliza Rais wa Marekani Joe Biden kwanini kuna mvutano katika uhusiano wa Uturuki na Marekani katika mkutano wa NATO.

 

Sabah: “'Utku' ilifanya kazi kwa mafanikio”

Rais wa Sekta ya Viwanda vya Ulinzi İsmail Demir, alisema kuwa UTKU, injini ya kwanza yenye nguvu ya horse power elfu moja na ya usafirishaji wa kwanza wa magari ya kivita ya uwezo wa kubeba hadi tani 45 za Storm Howitzer, ilifanya kazi kwa mafanikio.

 

Yeni Şafak: "Uwanja wa ndege wa Istanbul na THY zaongoza Ulaya kwa wiki kadhaa na idadi ya safari za ndege"

Kulingana na data ya Shirika la Usalama la Usafiri wa Anga la Ulaya, Uwanja wa ndege wa Istanbul na Shirika la ndege la Kituruki (THY) zimedumisha nafasi za uongozi wao barani Ulaya kwa idadi ya safari za ndege za kila siku. Kati ya Mei 16-30, Uwanja wa ndege wa Istanbul ulidumisha nafasi yake ya kwanza Ulaya na wastani wa safari 632 za ndege kwa siku. THY ilikuwa kileleni kwa safari 823 za ndege kati ya 24 na 30 Mei.

 

Star: "Oleskiv: Tunataka kutekeleza maombi ya cheti cha utalii nchini Uturuki"

Rais wa Wakala wa Maendeleo ya Utalii wa Ukraine Maryana Oleskiv alisema kwamba walipendelea ombi salama la hati ya utalii nchini Uturuki na akasema, 'Tulifanya mikutano ili kupata uzoefu juu ya uthibitisho kwa ajili ya Ukraine.'

 

Haber Türk: "Urusi imeongeza kiwango cha kuagiza nyanya kutoka Uturuki"

Kulingana na amri iliyoidhinishwa na Wizara ya Kilimo ya Urusi, kiwango cha nyanya kilichoagizwa na Urusi kutoka Uturuki kiliongezeka kwa tani elfu 50 hadi tani elfu 300.Habari Zinazohusiana