Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 06.04.2021

1615390
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Haber Türk: "Taarifa ya Erdoğan juu ya Montreux"

Rais Recep Tayyip Erdoğan alisema kwamba Uturuki imeona faida kubwa ya Mkataba wa Montreux Straits wa mwaka 1936, na wataendelea kuzingatia makubaliano haya kwa manufaa bora zaidi. Erdoğan alisisitiza kuwa iwapo uhitaji utajitokeza katika siku zijazo, hawatasita kupitia tena kila makubaliano ili kuifanya nchi iwe bora.

 

Star: "Simu ya Erdoğan kwa viongozi wawili"

Rais Erdoğan alizungumza kwa simu na Rais mteule wa Kosovo Vjosa Osmani-Sadriu na kutoa pongezi zake. Akigusia mtazamo wa kujenga wa jamii ya Uturuki katika kuanzishwa kwa serikali mpya na michakato ya uchaguzi wa Rais, Erdoğan alisisitiza kwamba anaamini kuwa uhusiano wa kihistoria na wa kindugu kati ya nchi hizo mbili utaimarishwa katika awamu mpya. Maswala ya pande mbili na ya kikanda pia yalijadiliwa katika mazungumzo ya simu kati Erdoğan na Amiri mkuu wa Qatar Al Sani.

 

Yeni Şafak: "Uturuki inaweza kufanya makubaliano ya anga na Urusi"

Mwenyekiti wa Shirika la Anga la Uturuki Hüseyin Yıldırım, alitangaza kuwa makubaliano ya karibu ya ushirikiano yatasainiwa na Urusi katika sekta ya anga. Yıldırım alisema, 'Tunaanzisha uhusiano na nchi na mashirika ya kimataifa ambayo tumeamua kulingana na malengo yetu ya kitaifa. Tunafanya kazi kwa ushirikiano na nchi nyingi, pamoja na Urusi, na tunapanga kutia saini makubaliano katika siku za usoni."

 

Vatan: "Ushirikiano mpya kati ya Uturuki na Azerbaijan"

Makubaliano mapya kati ya Uturuki na Azerbaijan yanatekelezwa juu ya kitambulisho cha usafiri. Kwa itifaki iliyosainiwa, jukwaa la pamoja la utalii haswa upande wa afya, litaweza kuundwa. Makubaliano haya yataongeza idadi ya ziara kati ya nchi hizo mbili.

 

Sabah: "Baada ya vyombo vya SİHA, lengo la sasa ni ndege za kivita zisizo na rubani"

Selçuk Bayraktar ametangaza mradi mpya baada vyombo vya anga vya SİHA vya Kituruki vilivyoonyesha mafanikio makubwa na kuchukuwa jukumu kubwa katika ushindi wa Azerbaijan kuikomboa Nagorno-Karabakh dhidi ya jeshi la Armenia mara ya mwisho. Bayraktar alisema shughuli inaendelea kwa ajili ya utengenezaji wa ndege za kivita zisizo na rubani.Habari Zinazohusiana