Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 04.03.2021

1594698
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Habari Türk: "Çavuşoğlu: Tunaweza kujadili mamlaka ya bahari na Misri"

Waziri wa Mambo ya nje Mevlüt Çavuşoğlu alisema kuwa kulingana na mwendo wa uhusiano kuhusu mamlaka ya baharini katika Mashariki ya Mediterania, mazungumzo yanaweza kufanywa na Misri. Waziri Çavuşoğlu alisema, "Tunaweza kutia saini makubaliano kati yetu baadaye."

 

Vatan: "Fuat Oktay: Tunatuma chanjo elfu 20 zaidi za Covid kwa KKTC wiki hii"

Makamu wa Rais Fuat Oktay alitoa maelezo katika mkutano na waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini (KKTC) Ersan Saner hapo jana katika mji mkuu wa Ankara, na kusema "Tunatuma chanjo elfu 20  zaidi kwa KKTC wiki hii. Kwa ujumla tutakuwa tumefikia elfu 100. Kwa hivyo, tutakuwa miongoni mwa nchi ya 1 u 2 duniani."

 

Star: "Shirika la kigaidi la PKK halipewi nafasi ya kupumua: 126 waliangamizwa"

Vikosi vya usalama vimefanikiwa kuendelea na operesheni zao dhidi ya shirika la kigaidi linalotenganisha la PKK / YPG. Magaidi 126 waliangamizwa katika operesheni dhidi ya shirika la kigaidi zilizoanzishwa ndani na nje ya nchi mnamo Februari 2021.

 

Sabah: "Toleo jipya la meli ya kivita ya Kituruki Cobra II iko tayari kwa huduma "

Otokar ambayo ni moja ya watengenezaji wa vyombo vya ardhini vya kivita vya tasnia ya ulinzi ya Uturuki, iliongeza mfumo wa "chombo cha ulinzi dhidi ya vilipuzi" kwa jamii ya bidhaa ya Cobra II. Sampuli ya toleo jipya la jamii ya vyombo vya kivita vya Cobra II 4x4 vinavyotumika katika nchi 15 ulimwenguni, iliundwa nchini Uturuki.

 

Hürriyet: "Msanii Bülent Evcil awekwa kwenye jalada la jarida maarufu la 'Falaut' la Italia"

Mkurugenzi wa Jimbo la Istanbul Symphony Orchestra (IDSO) na msanii wa filimbi Bülent Evcil, aliwekwa kwenye jalada la "Falaut", jarida maarufu la sanaa la Italia ambalo limekuwa likichapisha kwa zaidi ya miaka 30. Katika jarida hilo, Evcil ambaye alionyeshwa kama moja ya mpigaji filimbi anayeongoza ulimwenguni, alitajwa kushiriki matamasha ya usanii katika nchi tofauti kama Brazil, Marekani na Italia, na kusimuliwa mafanikio yake na tuzo mbalimbali alizopewa.Habari Zinazohusiana