Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Leo Katika Magazeti ya Uturuki

1383831
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Haber Türk: “Uturuki ni mfano wa kuigwa ulimwenguni kwa mshikamoano wake”

Waziri wa afya wa Uturuki Fahrettin Koca  akizungumza kuhusu virusi vya Covid-19 , amesema kuwa Uturuki ni mfano wa kuigwa kwa utofauti wake ulimwenguni.  Uturuki imechukuwa hatua zinazostahili  kabla ya janga la virusi hivyo kusababisha maafa makubwa. Uturuki imejali  hali iliopo katika jamii na kuchukua hatua zilizosambamba na  hali halisi katika maisha ya kila siku ya waturuki.  Hatua hizo zimepunguza kwa kiasi kikubwa athari ambazo zingesababishwa na virusi hivyo.  Tutawafahamisha kila siku  hali za waathirika zinavyozidi kubadilika na kuwa nzuri amesema Koca. Idadi ya wagonjwa wanaopona inaonesha matumaini.

Sabah: “Wito kwa vijana kutoka kwa waziri wa afya wa Uturuki”

Tumeanza mfumo mpya  wa maisha amesema waziri wa afya wa Uturuki Fahrettin Koca, akiwatolea wito vijana  kubaki majumbani mwao ili kujilnda na maambukizi ya virusi vya corona.  Katika ujumbe wake aliotoa katika ukurasa wake wa Twitter, waziri Koca amesema kuwa maisha ni harakati ila katika kipindi hiki kigumu tumelazimika kabaki majumbani mwetu ili kupunguza kiwango cha mambukizi na  kuwapunguzi kazi wauguzi na madaktari.

Hürriyet: “Watalii waliopo nchini Uturuki hawataki kurejea katika mataifa yao"
 Mataifa mengi  ulimwenguni yameweka sheria kali  kutokana na janga la virusi vya corona. Baadhi ya mataifa  yamefunga  utalii. Kutokana na hali nzuri iliopo Uturuki, watalii wengi wameonesha   kutaka kuendelea kuishi nchini Uturuki. Huduma na mapokezi kwa watalii Uturuki ni bora kuliko katika mataifa mengine.

Yeni Şafak: “madakatari  wa Syria :  tuna haki ya kupambana na virusi vya corona"
Madaktari  kutoka Syria waliokimbizi mauaji  na kupewa hifadhi Uturuki wapo zaidi ya 100  mkoani Gaziantep amefahamisha kuwa nao wana haki ya kuonesha  mchango wao katika  juhudi za mapambano dhidi ya virusi vya corona na kuwa bega kwa bega na Uturuki katika kipindi hiki kigumu.Muakilishi wa madakatari kutoka Syri Daktari  Mustafa Lulik  amesema kuwa tangu mwaka  2011 tumeonesha ushirikiano na tunahitaji  kuwa karibu ya watu walioathirika kutoa mchango wetu.

Vatan: “Kiwango cha matumizi chaongezeka”

Kiwango cha  matumizi chaongezeka kwa asilimia  1,7 iklinganishwa na mwezi uliopita.  Februari ilikuwa asilimia  57,3 na Machi asilimia  58,2.
 Habari Zinazohusiana