Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Leo Katika Magazeti ya Uturuki

1383280
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Hürriyet: "Ujumbe wa sauti kutoka kwa rais Erdoğan kwa raia wake"
Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan atoa ujumbe wa sauti kwa raia wake kuhusu tahadhari zilzitolewa kuhusu virusi vya  corona. 
 Rais Erdoğan amewatahadhari watu wanaoshinda kubaki majumbani kwao kwa kuwaambia kuwa wanahatarisha maisha yao na kuwatolea wito wa  kubaki majumba kwao ili  kukabiliana na virusi hivyo.

Vatan: "Fahrettin Altun: Habari kuhusu Covid-19 katika mitandao ya kijamii ni hatari kuliko virusi vyenyewe "
Muhusikwa  katika katika kitengo cha mawasiliano nchini Uturuki Fahrettin Altun awatahadharisha raia na habari kuhusu virusi vya corona vinazotolewa katika mitandoa ya kijamii na kusema kwamba habari hizo ni hatari kuliko virusi vyenyewe. Altun ameomba raia kufuatilia habari zinazotolewa na kurasa  rasmi zinazohusika na habari kuliko kuamini kila kinachopeperushwa katika mitandoa ya kijamii.  Altun ametoa ujumbe huo kupitia video na kukumbusha uhatari wa virusi hivyo.

Sabah: " Uturuki yaingiza kiwango cha dola bilioni 42 katika utenegenzaji wa barabara"
Mkurugenzi katika shirika la UND la kimakati  Fatih Şener amesema kuwa Uturuki imeingiza kiwango cha dola  bilioni 42 katika ujenzi wa barabara kwa mwaka mmoja.

Haber Türk: "Mauzo ya nje ya matunda yaongezeka Uturuki"
Kiwango cha mauzo ya nje ya matunda na mboga za majani chaongezeka kwa asilimia 27,6  Uturuki ikilinganishwa na kipindi kama hicho kati ya Januari mosi  hadi Machi 19 mwaka uliopita na mwaka 2020.Habari Zinazohusiana